BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HALI YA HEWA YATABIRI MVUA NYINGINE KUBWA LEO, HII MIKOA HUENDA IKAATHIRIKA.


Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam  siku wakichimba udongo chini ya Daraja la Mto Msimbazi lililopo Tabata Matumbi jana kutafuta miili ya ndugu zao waliozolewa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya jiji. Picha na Venance Nestory.

DAR ES SALAAM. 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa kunyesha tena kuanzia leo na kesho katika ukanda wa Pwani.
Katika taarifa yake kwa umma jana jioni, TMA imesema maeneo ambayo yataathiriwa na mvua hizo za kuanzia leo ni Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na mikoa ya Tanga, Pwani na Dar es Salaam.
Huo ni mwendelezo wa mvua zilizosababisha maafa makubwa ambazo zilianza kunyesha Aprili 10, mwaka huu katika ukanda huo wa pwani. Maeneo yaliyokuwa yameathiriwa zaidi ni Dar es Salaam na Morogoro ambako zaidi ya watu 25 walifariki dunia.
Mbali ya vifo hivyo, mvua hizo zilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara hasa madaraja.
Mawasiliano ya barabara kati ya Mkoa wa Dar es Salaam na mingine nchini yalikatika kwa siku mbili baada ya barabara zake zote zinazouunganisha na maeneo hayo ama kuharibiwa vibaya na mafuriko au kujaa maji na kushindwa kupitika.
Taarifa hiyo ya TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kuwa kubwa kwani zitazidi milimita 50 katika saa 24.
“Wakazi wa maeneo hatari, watumiaji wa bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki,” ilisema taarifa hiyo.MWANANCHI

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: