BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAANDISHI WA HABARI MAGAZETI YA MWANANCHI, NIPASHE NA HABARILEO WATWAA TUZO ZA ULUGURU AWARD 2013-2014 MOROGORO.

Mwandishi Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Juma Mtanda kushoto Mwenyekiti wa Morogoro Press Club na Mwandishi Mtangazaji wa Nipashe na Redio One, Idda Mushi (katikati) na John Nditi wa Habarileo kulia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutwaa tuzo bora za uandishi bora za Uluguru award 2013-2014 zilizoandaliwa na kituo cha Maendeleo na Utamaduni katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mambo Club April 12 mwaka huu.PICHA ZOTE/MTANDA BLOG.

Idda Mushi akionyesha tuzo yake, kushoto ni mgeni rasmi Joel Bendera ambaye ni mkuu wa mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera kushoto akimkabidhi tuzo mwandishi mpigapicha wa kampuni ya Mwananchi Communition Ltd Morogoro, Juma Mtanda baada ya kushinda tuzo ya Uluguru Award 2013-2014, lengo likiwa ni kuchochea uajibikaji kwa kufuata misingi ya utawala bora katika nyanja mbalimbali iliyoandaliwa na Kituo cha Maendeleo ya Utamaduni (Kimau) kutokana na mchango katika kuripoti baadhi ya habari za migogoro ya wakulima na wafugaji, mafuriko yaliyowakumba wananchi wa la kijiji cha Magole yaliyotokea hivi karibuni katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mambo Club Morogoro.

John Nditi akionyesha tuzo yake baada ya kukabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro kushoto.
Huyu ni Cosma Cheka naye alitwaa tuzo kwa upande wa bondia aliyetwaa mataji mawili ya mchezo huo.
Mkurugenzi wa matawi ya benki ya CRDB, Nelie  Ndosa akitwaa tuzo
Mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi Lilian Lucas Kasenene kulia akina na Juma Mtanda baada ya kutunuziwa tuzo hiyo.
Safu ya viongozi wa CRDB, ikiongozwa na Mkurugenzi wa matawi ya benki ya CRDB, Nelie  Ndosa na mkurugenzi wa CRDB, Pendo Asay kushoto baada ya kutwaa tuzo ya taasisi bora ya kifedha ya mwaka 2-13-2014.
Mkurugenzi wa kituo cha Maendeleo na Utamaduni, Anthony Mhando kulia akimkabidhi tuzo mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera kufuatia tuzo ya kiongozi bora.
Mkurugenzi wa kituo cha Maendeleo na Utamaduni, Anthony Mhando
Sehemu ya waalikwa wa hafla ya tuzo hizo

Mkurugenzi wa kituo cha Maendeleo na Utamaduni, Anthony Mhandokulia akifafanua jambo kwa Bendera kushoto na Mourice Massala (katikati) muda mfupi kabla ya kuanza hafla hiyo.





Mwandishi wa Jamboleo Peter Kimath (katikati) akiwa na mtangazaji wa kituo cha redio cha Planet FM Morogoro, Walda Makongwa kushoto na ndugu yao kulia wakati wa tuzo hizo.
John Nditi akiwa na wadu mbalimbali wa tuzo hizo
Katibu wa mbunge wa jimbo la Morogoro, Mourice Massala akizungumza jambo baada ya ofisi ya mbunge wa jimbo hilo kutwaa tuzo bora katika nyanja ya kiongozi bora.
 

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo, kushoto ni Mkurugenzi wa kituo cha Maendeleo na Utamaduni, Anthony Mhando.

Na Lilian Lucas, Morogoro.
Watu kadhaa akiwemo mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Juma Mtanda ametunukiwa  tuzo ya heshima ya Uluguru Award ya mwaka 2013/14, kuhusu uandishi wa habari na upigaji picha za matukio mbalimbali yanayogusa jamii, mkoani Morogoro.

Tuzo hiyo imetolewa na Kituo cha Maendeleo ya Utamaduni cha mjini Morogoro (Kimau).

Akitangaza tuzo zilizotunukiwa kwa taasisi mbalimbali, Mkurugenzi wa kituo hicho, Morogoro Anthony Mhando, alisema lengo ni kuchochea uajibikaji kwa kufuata misingi ya utawala bora katika nyanja mbalimbali.

Mhando alizitaja nyanja hizo kuwa ni pamoja na uandishi wa habari zinazogusa jamii, ujasiriamali, uwekezaji, utawala bora, michezo na usanii.

Mhando aliwataja washindi wa tuzo hizo kuwa ni pamoja na mpigapicha wa gazeti la mwananchi mkoa wa Morogoro, Juma Mtanda aliyetwaa tuzo hizo kutokana na mchango katika kuripoti baadhi ya habari za migogoro ya wakulima na wafugaji, mafuriko yaliyowakumba wananchi wa la kijiji cha Magole yaliyotokea hivi karibuni.

Wengini waliotwaa tuzo ya uandishi wa habari ni Mwandishi Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha ITV ambaye ni Mwenyekiti wa Morogoro Press Club, Idda Mushi, John Nditi kutoka TSN na Walda Magongwa wa kituo cha redio cha Planet FM.

Kwa upande wa viongozi utawala bora ni mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood,  mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera huku ngazi ya wajasiliamali, Bacho Sadik Bacho ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA) akitwaa tuzo hiyo. Alisema Mhando.

Kwa upande wa taasisi za kifedha CRDB yenyewe iliibuka na tuzo ya taasisi bora ya kifedha huku kampuni ya uwekezaji kiwanda cha kusindika tumbaku (TLTC) wakitwaa tuzo ya kampuni bora wakati kwa upande wa michezo, jina la Shomari Kapombe likiibuka katika soka, Cosmas Cheka ambaye ni mwanamasumbwi, Azack Sokas aliyetwaa tuzo kupitia mchezo wa kareti.

Viongozi wa michezo ni Zumo Makame, Awadh Komba na Paschol Kianga ambaye ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) kwa wasanii Miss Tanzania 2013 Happness Watimanya na Afande Sele anayejisghuhulisha na muziki wa kizazi kipya huku mkuu wa mkoa wa Morogoro akiwa mgeni rasmi katika haflas hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mambo Club.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: