BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PALESTINA IPO TAYARI KUSITISHA MAPIGANO UKANDA WA GAZA NA ISRAEL.

Uharibifu uliofanywa Gaza kutokana na vita.

Uongozi wa Palestina umependekeza makubaliano ya saa ishirini na nne ya kusitisha mapigano dhidi yake na Israel.
 
Yasser Abed Rabbo wa chama cha PLO, Palestine Liberation Organisation amesema mpango huo umeungwa mkono na makundi muhimu likiwemo kundi la Hamas na la Islamic Jihad.


Hata hivyo mmoja wa maafisa wa Hamas Abu Zuhri amesema taarifa hiyo ya PLO haiwakilishi upande wa Hamas.


Mapema pendekezo la makubaliano ya kusitisha mapigano lililotangazwa, halikuweza kutekelezwa kwa kuwa hakuna upande wowote ulioweza kulitekeleza kwa kusitisha mapigano katika eneo la Gaza.


Bwana Rabbo amesema ujumbe wa pamoja unaoongozwa na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas utakwenda Cairo kuweka masharti ya kusitisha mapigano.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: