BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ASKOFU !!! ACHA BUNGE LA KATIBA MAALUMU LIMAZIKE MAANA HALINA MAANA KABISA.


Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini.

Mwanza.
Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amesema Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea halina maana yoyote hivyo liachwe limalize muda wake.

Akizungumza kwenye mahojiano juzi, Askofu Kilaini alisema mpaka sasa malengo ya Bunge hilo hayajajulikana, hivyo hakuna haja ya wananchi kulumbana na wajumbe hao kwa sababu fedha zilizotumika hazitarudishwa.


“Kama ni fedha zimeshaliwa nyingi tu siku zilizobaki ni chache, Katiba wanayopitisha ni ya wananchi siyo ya Bunge. Lenyewe (Bunge) linapendekeza tu, hivyo hata wakatengeneza rasimu yao si lazima ipitishwe na wananchi,” alisema Askofu Kilaini na kuongeza:


“Wakiweza kuwafanya wananchi waikubali basi hapo maana yake ni nzuri, kitu ambacho ni kigumu kutokea. Tuwaache wamalize muda wao hakuna sababu ya kuleta vurugu kwa sababu ya hilo.”


Alisema jambo muhimu kwa sasa ni kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na ule mkuu mwakani uwe wa haki, washiriki waridhike na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Rais Kikwete na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) yamesaidia.


“Rais (Jakaya Kikwete) amefanya uamuzi wa busara kuahirisha Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu hatima yake haiwezi kupatikana Katiba Mpya kipindi hiki kifupi.



Tumejaribu kipindi cha kwanza lakini ni bora kuruhusu uchaguzi mkuu, hili ni muhimu la kuzingatia. Hatutakuwa wa kwanza kuahirisha mchakato huu kwa sababu Kenya, Afrika Kusini hata Marekani wamefanya hivyo kwa mara nyingi,” alisema Kilaini na kuongeza:


Askofu Kilaini alisema mambo muhimu kwake ni uwapo wa Tume Huru ya Uchaguzi, Mgombea binafsi ingawa kwa sasa kushinda urais itakuwa ni vigumu.

lakini anaweza kuleta usawa kwa wanaoteua kwenye vyama vyao wawe makini.
“Rais mpya apate walau asilimia 50 kwa sababu chini ya hapo anakuwa rais dhaifu sana, waliochaguliwa kama wapinzani hawaridhiki kesi ziende mahakamani. Kwangu mimi nakubali ngazi nyingine isipokuwa ya urais,” alisema Askofu Kilaini.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: