BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MICHEZO YA COPA COCA COLA 2014 YAANZA KUTIMUA VUMBI UWANJA WA SABASABA MANISPAA YA MOROGORO

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanga U17, Issa Bakari akitafuta mbinu ya kumiliki mpira dhidi ya mchezaji wa Dodoma, Fullgence Tambo na Braka Kadeti wakati wa mchezo wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 kituo cha Morogoro katika uwanja wa jamhuri ambapo katika mchezo huo Tanga ilitandikwa bao 1-0.Picha ya Maktaba Mtanda Blog.

Na Mtanda Blog, Morogoro.
Mashindano ya Copa Coca Cola 2014 chini ya umri wa miaka 15 yameanza kutimua vumbi katika uwanja wa Sabasaba kwa kushirikisha jumla ya timu tano ambayo yatatoa nafasi kwa makocha kuteua wachezaji wataounda kikosi cha umri huo kwa ajili ya kuwakirisha mkoa wa Morogoro katika mashindano hayo ngazi ya taifa hapo baadaye.


Katibu mkuu mtendaji wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka alieleza kuwa hapa kuwa mashindano ya copa coca cola 2014 chini ya umri wa miaka 15 yanaanza kutimu vumbi leo Septemba 17 katika uwanja wa Sabasaba ikishirikisha timu tano.

Semka alitaja timu hizo kuwa ni pamoja na Morogoro Vijijini, Manispaa, Mvomero, Kilosa na Kilombero huku Ulanga ikishindwa kuleta timu kutokana na sababu mbalimbali za kiuongozi.

“Copa coca cola 2014 chini ya umri wa miaka 15 yanaanza kuchezwa leo katika uwanja wa Sabasaba kuanzia saa 3 asubuhi na saa 10 jioni na haya mashindano safari hii yanashirikisha timu za wilaya tano tu, kwanzi ndizo zilizothibitisha kuleta timu isipokuwa Ulanga wameshindwa kuleta timu pamoja na Gairo.”alisema Semka.

Semka alisema kuwa michezo hiyo inafanyika kwa siku mbili ambapo kila siku kutakuwa na michezo mitano na katika siku hizo jopo la walimu watakuwa na kazi ya kuteua wachezaji wa kuunda kikosi kitakacho wakilisha mkoa wa Morogoro katika mashindano ya copa coca cola ngazi ya taifa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: