BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

REAL MADRID YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA ULAYA IKIPATA USHINDI WA BAO 5-1, ARSENAL KIMEO.



Hatimaye ligi ya mabingwa wa ulaya imeanza tena kwa michezo kadhaa kupigwa usiku wa jana huku mabingwa wa watetezi Real Madrid wakianza kuutetea ubingwa wao kwenye mchezo dhidi ya FC Basle.

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu umeisha kwa matokeo ya ushindi mzito kwa Real Madrid walioibamiza Basle 5-1.

Suchy alianza kujifunga goli kwenye dakika ya 14 na kuipa uongozi Madrid, kabla ya Gareth Bale kufungua ukurasa wake wa magoli kwenye UCL kwa kufunga goli la dakika ya 30, Cristiano Ronaldo akaongeza lingine dakika ya 31, James Rodriguez akafunga goli la 4 dakika ya 36, na Karim Benzema akashindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la FC Basle dakika ya 79.

Timu zilipangwa hivi:
Real Madrid: Casillas, Pepe, Sergio Ramos, Marcelo, Nacho, Kroos, Rodriguez, Bale, Modric, Ronaldo, Benzema.
Subs: Navas, Varane, Fabio Coentrao, Hernandez, Arbeloa, Isco, Illarramendi.
Goals: Suchy OG 14, Bale 30, Ronaldo 31, Rodriguez 36, Benzema 79

Basle: Vaclik, Samuel, Schar, Suchy, Safari, Zuffi, Frei, El-Nenny, Xhaka, Streller, Gonzalez.
Subs: Vailati, Delgado, Gashi, Kakitani, Aliji, Embolo, Calla.
Goal: Gonzalez 37
Referee: Damir Skomina (Slovenia)
Liverpool 2-1 Ludogorets Champions League.

Baada ya kukosa michuano ya ulaya kwa misimu kadhaa hatimaye klabu ya Liverpool jana ilirejea rasmi kwenye michuano hiyo wakianza kutupa karata yao ya kugombea ubingwa huo kwa kucheza dhidi ya Ludogorets.

Mechi hiyo iliyomalizika dimba la Anfield ilikuwa ngumu huku wageni wakionekana kuwasumbua sana wenyeji.

Lakini magoli mawili ya mshambuliaji mpya wa Liverpool Mario Balotelli na nahodha Steven Gerrard yalitosha kuwapa Liverpool ushindi wa kwana kwenye hatia ya makundi ya michuano hiyo.

Balotelli alifunga goli dakika ya 81, kabla ya goli hilo kisawazishwa na Dani Abalo dakika chache baadae, lakini huku zikiwa zimeongezwa dakika 2 Steven Gerrard akaiweka kambani penati yake na kuipa ushindi timu yake, 

Liverpool: Mignolet 6; Manquillo 6, Lovren 6.5, Sakho 6, Moreno 7.5; Henderson 7, Gerrard 7, Lallana 6 (Borini 67, 6); Sterling 7, Coutinho 5 (Lucas 67, 6), Balotelli 5.
Subs: Brad Jones, Jose Enrique, Toure, Lambert, Suso.
Scorers: Balotelli, 81, Gerrard (pen), 90+2

Ludogorets: Borjan 6; Caicara 6, Moti 6.5, A Aleksandrov 6, Minev 6.5; Dyakov 7, Abel 7; M Aleksandrov 6.5, Marcelinho 6.5, Misidjan 6; Bezjak 6.

Subs: Gospodinov, Fabio Espinho, Angulo, Dani Abalo, Zlatinski, Wanderson, Younes.
Scorers: Dani Abalo.
Referee: Matej Jug (Slovenia).

Arsenal yaambulia kipigo kutoka kwa Dortmund kwa kufungwa bao 2-0 nchini Ujerumani.

Katika mchezo mwingine wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa ulaya, klabu ya Arsenal jana ilikaribishwa na Borrusia Dortmund katika mchezo wa kwanza wa kundi D.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa BVB – Signal Iduna Park, uliisha kwa Arsenal wakipokea kipigo cha kwanza kwenye michuano baada ya kutandikwa bao 2-0.

Cirro Immobile alianza kuifungia Dortmund katika kipindi cha kwanA kabla ya Pierre-Emerick Aubameyang kufunga goli la pili dakika ya 48.

Danny Welbeck itabidi ajilaumu mwenyewe kutokana na kupoteza nafasi 3 za wazi za kufunga kwenye mchezo.

Arsenal mechi ijayo watacheza na Galatasary ambao leo hii nao waliotoka sare dhidi ya Anderletch.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: