BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TISHIO LA EBOLA LAIKUMBA TANZANIA, NI NCHI 15 YENYE HATARI YA KUKUMBWA KUTOKANA NA MAELEZO YA WANASAYANSI.


Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la Citizen toleo la jana, mamlaka zilizoko chini ya Wizara ya Afya zimeendelea kukabiliana na hofu ya kuibuka kwa ugonjwa huo hatari uliozikumba nchi nyingi za Afrika Magharibi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000.


Dar es Salaam.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 15 zilizoko katika hatari ya kupata mlipuko wa ugonjwa wa ebola kwa mujibu wa maelezo ya wanasayansi.

Wanasayansi hao wa Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza pia wameainisha kuwa zaidi ya watu milioni 22 barani Afrika wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.


Hadhari hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Serikali ikiwahakikishia wananchi wake kwamba iko katika jitihada ya kuandaa mazingira ya kukabiliana na ugonjwa huo endapo utaingia nchini.


Wakati wanasayansi hao wakisema hayo, wiki iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alikagua maandalizi ya kituo cha kupokea wagonjwa wa ebola eneo la Temeke na mitambo iliyowekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) endapo watapatikana wasafiri wenye dalili za maradhi hayo.


Vilevile kuona jinsi wahusika walivyopewa mafunzo maalumu ya kuwahudumia wagonjwa hao.


Tayari mitambo hiyo imeshafungwa katika Viwanja vikubwa vya ndege vya Kilimanjaro (KIA), JNIA, Uwanja wa Ndege wa Zanzibar na Uwanja wa Ndege wa Mwanza.


Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la Citizen toleo la jana, mamlaka zilizoko chini ya Wizara ya Afya zimeendelea kukabiliana na hofu ya kuibuka kwa ugonjwa huo hatari uliozikumba nchi nyingi za Afrika Magharibi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000.


Iwapo kutakuwa na taarifa zozote za kuibuka kwa ugonjwa huo, tayari kambi maalumu za kuwatambua wagonjwa wa ebola zimeshaanzishwa katika Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi cha Muhimbili ambako watafanyiwa uchunguzi na watakaobainika watapelekwa katika kituo maalumu cha kuwahifadhi kilichoko katika Hospitali ya Temeke.


Kengele ya hatari
Ugunduzi mpya uliofanywa katika eneo ambalo ebola imeonyesha athari kubwa Afrika Magharibi umezidi kutoa ishara ya hatari kwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika ambazo mlipuko haukuwahi kuripotiwa.


Serikali za nchi hizo zimehadharushwa kuwa zinatakiwa zijipange kwa kujua njia na namna ya kukabiliana na tishio hilo badala ya kuelekeza nguvu katika kuwabaini waathiriwa kupitia viwanja vya ndege na bandari pekee.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: