BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TBC1, JESHI LA POLISI INAPOINGIA KATIKA DOA KUWA ADUI MKUBWA WA DEMOKRASI NA UTAWALA BORA TANZANIA.


Kwa ufupi.
Matokeo ya ukiritimba wa TBC1 ni kuwa inaendelea kukosa watazamaji kwa sababu inafanya propaganda za kisiasa za chama tawala. Leo ukiangalia kinachoongelewa kwenye vyombo vya habari vya serikali ni mambo ya Chama cha CCM zaidi kuliko habari za kitaifa.


Wahenga husema “kikulacho ki-nguoni mwako.” Serikali ya Tanzania imejipambanua na kujipigia debe kama ni serikali inayoongoza kwa kutumia demokrasia na utawala bora. Kusema ni rahisi kuliko kutenda, Watanzania wa leo wanataka kuona vitendo zaidi kuliko porojo hasa wakizingatia kwamba “ maneno matupu hayawezi kubadilisha maisha ya wananchi maskini wa Tanzania,” hasa baada ya miaka zaidi ya 50 ya uhuru.



Demokrasia inatafasiriwa kama ni “utawala wa watu kwa ajili ya watu wale wale” ili kuweza kujiongoza katika misingi ya haki, amani, umoja, upendo, mshikamano na kustawisha jamii husika.


Viongozi wa kidemokrasia ni sharti wachaguliwe na watu wenyewe kwa kutumia mfumo ulio wazi na unaokubalika na wananchi wenyewe. Demokrasia inadai uhuru, haki, na mazingira sawa hasa katika nyakati hizi za vyama vingi vya kisiasa kama ilivyo Tanzania.


Je, nchi yetu ya Tanzania demokrasia leo ipo au haipo? Kama kuna demokrasia kwa nini serikali inatumia mfumo wa zamani katika kuendesha chaguzi zake ziwe ndogo au kubwa?


Kwa nini serikali ya CCM inaogopa kubadilisha sheria za uchaguzi ambazo zilikuwa ni za chama kimoja na sasa tupo katika mfumo wa vyama vingi?


Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusu demokrasia ya Tanzania katika dunia hii ya siasa za vyama vingi.


Leo kinachoonekana katika siasa za Tanzania ni hiki kwamba ‘adui mkubwa wa ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania ni vyombo vya dola.


Serikali ya CCM imejitahidi sana kutaifisha na kuhodhi vyombo vyote hata vile vilivyotakiwa kutumiwa na jamii kama televisheni ya taifa maarufu kama TBC1.


Chombo hicho cha habari cha umma kinaendeshwa kwa kutumia kodi za wananchi wote bila kujali dini, chama cha siasa, kabila na hivi kinatakiwa kihudumie wananchi wote. Inatia aibu kuona chombo cha Taifa kinafanya upendeleo wa wazi katika kutoa huduma zake.


TBC1 inatakiwa iwe huru katika utendaji wake bila kuminya uhuru katika utendaji wake. Matokeo ya ukiritimba wa TBC1 ni kuwa inaendelea kukosa watazamaji kwa sababu inafanya propaganda za kisiasa za chama tawala. Leo ukiangalia kinachoongelewa kwenye vyombo vya habari vya serikali ni mambo ya Chama cha CCM zaidi kuliko habari za kitaifa.


Chombo kingine ambacho kimekuwa ni kikwazo kwa ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania kwa muda mrefu tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi ni Jeshi la Polisi.


Hakuna Mtanzania mwenye akili asiyefahamu kwamba jeshi hilo la polisi sasa linaitwa “poliCCM’ kwa maana kwamba linafanya kazi ya kwa masilahi ya CCM. Hii ni aibu kubwa sana, kwa sababu nalo linatumia kodi za wananchi ambao wapo katika vyama vingi, na hivi kupaswa kufanya kazi bila upendeleo hasa ule wa kukibeba chama hicho tawala kwa kisingizio cha ‘kulinda amani na utulivu” ambavyo haviko.


Mara nyingi polisi wameonekana ndiyo wasabaishaji wa vurugu katika mikutano ya kisiasa hasa ya wapinzani.


Chombo kingine ambacho ni cha dola na kinachoendelea kuwa adui mkubwa wa demokrasia na ustawi wake nchini Tanzania ni Tume ya Uchaguzi. Tume hii imekuwa ikilalamikiwa kila uchaguzi tangu kurejeshwa kwa mfumo kwa vyama vingi nchini.


Ndiyo maana ninaandika na kuamini kwamba “ adui mkubwa wa ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania ni vyombo vya dola.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: