BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ULEMAVU WA TANZANIA IPO SIKU WATATOWEKA.


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi (kushoto), akisalimiana na watu wenye ulemavu wakati wa ufunguzi wa tamasha la tatu la watu wenye ulemavu Tanzania linalohusu `Ushiriki wa watu wenye ulemavu katika michakato ya kidemokrasia' lililofanyika jijini Dar es Salaam jana. PICHA: OMAR FUNGO.


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, amesema ana ndoto kwa Tanzania kufikia wakati asasi za watu wenye ulemavu kutoweka kabisa na kila mmoja atathaminiwa kwa utu wake.

Dk. Mengi aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa tamasha la tatu la watu wenye ulemavu Tanzania jijini Dar es Salaam jana.

Alisema katika suala la uumbaji hakuna awezaye kuhoji uumbaji wa Mungu. “Lazima tufahamu kuwa sisi tuliowazima ni walemavu watarajiwa, hivyo si vizuri walemavu kuomba miundo mbinu ya maeneo ya huduma za jamii kuboreshwa kwa kuwa hiyo ni haki yao,” alisema.

Dk. Mengi alisema walemavu wanapaswa kutembea kifua mbele kwa kutambua kuwa Mungu aliwaumba kwa makusudi na kamwe wasikubali kuitwa namba mbili na kuwa wanyonge bali wakubali kuitwa namba moja.

Pia Dk. Mengi aliwaambia washiriki kuwa mawazo yao hayatachukuliwa kama ya watu wenye ulemavu bali yatachukuliwa kama mawazo ya Watanzania wasio na ulemavu.

Wakati huo huo, Dk. Mengi aliwataka washiriki wa tamasha hilo wasikubali kurubuniwa kwa rushwa, wakikubali kununuliwa watakapoingia bungeni au kwenye madaraka watajali maslahi yao.

Alisema hawakuwa na ari ya kuwasaidia watu wenye ulemavu, hivyo itakuwa vigumu kupiga vita rushwa, uovu na umaskini katika jamii.

“Kupiga kura ni haki ya kikatiba kwa kila Mtanzania, lakini walemavu wamekuwa na mahitaji maalumu ambayo hayajafanyiwa kazi kisera au kisheria, sera na sheria zinapaswa kuleta mabadiliko yanayowajali walemavu,” alisema.

Mkurungenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society (FCS), John Ulanga, alisema taasisi yake imetumia Sh. bilioni 8.3 kwa ajili ya kusaidia asasi za kiraia za watu wenye ulemavu, ikiwamo miradi 447.

Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania (Chawata), John Ulabu, alimshukuru Dk. Mengi kwa juhudi zake kuwasaidia watu wenye ulemavu na kuwaomba wadau wengine wamuunge mkono.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: