BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAFANYAKAZI 1,500 WA SHIRIKA LA RELI KULIPWA MAMILIONI YA VIJISENTI BAADA YA TUME YA USULUHISHI NA MIGOGORO YA KAZI KUPITA TAFU.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUShRieDt-cnlP7FzaxLlW1eW5e__XSwVC-pTCbmiQJXmV63XT4gnCZMBdpMFR440DvDqr8BlbyIG-RoIVN97tCYHqAU6HigD3YLMWwkfy6HwwQeZbZc0EeA-EZtep4A1TILsIN3OCrX0/s1600/ABIRIA+WAKIDANDIA+TRENI.jpg
TUME ya Usuluhishi na Migogoro ya Kazi (CMA) imelitaka Shirika Hodhi la Reli (RAHCO) la mali zilizokuwa chini ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuwalipa mafao yao wafanyakazi 1,500 waliokuwa wameajiriwa na TRC, kabla ya mkataba baina yao na shirika hilo kukoma.

Uamuzi wa tume hiyo umetolewa mjini Tabora na Mwenyekiti wa CMA, Adolf Anosisye. Katika uamuzi huo, Mwenyekiti huyo wa CMA ameipa siku 90 RAHCO kutekeleza uamuzi huo wa kushughulikia mafao hayo ya wafanyakazi hao wa iliyokuwa TRC.

Anosisye alisema amefikia uamuzi huo, baada ya kupitia vielelezo mbalimbali vilivyowasilishwa kwenye tume hiyo na pande mbili zinazosigana kwenye mgogoro huo.

Alisema RAHCO inawajibika kisheria kushughulikia malipo ya wafanyakazi hao na kuwalipa mafao yao ya kustaafu. Madai ya msingi, yaliwasilishwa kwenye tume hiyo na Japhet Mkoba kwa niaba ya wafanyakazi 1,500 waliokuwa waajiriwa wa TRC.

Katika madai hayo, wafanyakazi hao wanaitaka Tume kutoa maamuzi ya kisheria ya kulipwa mafao yao na RAHCO, ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia ufilisi wa mali na madeni ya TRC.

Mkoba na wenzake, katika madai yao hayo, wanadai walipwe jumla ya Sh bilioni 16.2 na lililokuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) baada ya mkataba wa utumishi baina yao na shirika hilo kukoma mwaka 2007, hivyo madai yao ya kulipwa mafao ya mwisho ya utumishi wao kuachwa mikononi mwa RAHCO.

Akizungumza na gazeti hili, Mkoba alisema kuwa waliamua kufungua mashauri katika Tume hiyo ya Usuluhishi baada ya kupigwa danadana na RAHCO na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), ambao kila moja ilikuwa ikisukuma jukumu hilo kwa mwingine.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: