BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU 40 WAWEKWA KALANTINI BAADA YA KUWA KARIBU NA MTOTO ALIYEAMBUKIZWA NA VIRUSI VYA EBOLA AKITOKEA GUINEA NCHINI MALI.

Ebola Kid.

Shirika la afya duniani WHO linasema kwa msichana wa umri wa miaka miwili ambaye alithibitishwa kuwa mgonjwa wa kwanza wa ebola nchini Mali alisafiri kilomita kadha kwa basi nchini humo huku akionyesha dalili za kuugua ugonjwa huo.

Zaidi ya watu 40 ambao walikaribiana naye wametengwa. Huenda msichana huyo alisafirishwa kwenda nchini Mali na nyanyake baada ya mazishi ya mamake nchini Guinea moja ya nchi ambazo zimeathirka pakubwa na ugonjwa wa ebola.

Utawala nchini Mali sasa umethibitisha kuwa msichana huyo ameaga dunia kwenye hospitali moja mjini Mayes alikokuwa akipewa matibabu.

Mwandishi wa BBC anayehusika na masuala ya afya anasema kuwa huenda ikawa changamoto kubwa kuwapata watu wengine ambao walikaribiana na msichana huyo.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: