BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JESHI LA POLISI LAZUIA MAZISHI YA AISHA MADINDA, KIFO CHAKE CHAKUMBWA NA UTATA, DAR ES SALAAM


AISHA MADINDA.

Dar es Salaam.
Jeshi la polisi limezuia mazishi ya aliyekuwa mnenguaji wa Twanga Pepeta na Extra Bongo, Aisha Madinda hadi hapo mwili wake utakapofanyiwa uchunguzi kutokana na utata wa kifo chake.


Akizungumza na Mwananchi, dada wa marehemu, Hamida Mbegu alisema Polisi waliwaambia kuwa mwili huo unahitaji kufanyiwa vipimo ili kubaini sababu za kifo chake, japokuwa familia haikuwa tayari kwa jambo hilo.


Alisema Polisi walisisitiza kuwa ni lazima mwili ufanyiwe vipimo kutokana na kuwapo kwa utata wa kifo hicho.


Hamida amesema kwa mujibu wa polisi vipimo vitafanyika asubuhi, hivyo baada ya vipimo kumalizika mwili utapelekwa Kigamboni ambako ndiyo familia imekusanyika na baada ya swala ya Ijumaa utazikwa kwenye makaburi ya familia yaliyopo Kibada, Kigamboni.


Akizungumzia suala hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura, alisema kuwa kutokana na mazingira ya kifo hicho ni lazima Polisi wajiridhishe kwa kuufanyia mwili vipimo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: