BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAJAMBAZI SITA YAHUKUMIWA ADHABU YA KUNYONGWA HADI KUFA NA MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM.


Utulivu mahakamani


Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa sita katika kesi ya mauaji ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wa mkoani Morogoro na mfanyakazi wa Benki ya NMB.



Mauaji hayo ambayo yalipata umaarufu na kupewa jina la mauaji ya Ubungo Mataa yalifanyika Aprili 20,2006 jijini Dar es Salaam.


Jaji Projest Rugazia amewataja washtakiwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa kuwa ni Mashaka Pastory, John Mndasha, Martine Mndasha, Haji Kiweru, Wycliff Imbora na Rashidi Abdikadir.


Jaji Rugazia anasema aliwatia hatiani washtakiwa hao na kuwahukumu kunyongwa hadi kufa, kufuatia ushahidi ulitolewa na mashahidi 29 wa upande wa mashtaka pamoja na vielelezo 78 vilivyowasilishwa mahakamani hapo na ushahidi wa utetezi.


“Maungamo ya washtakiwa, ushahidi wa kitaalam na utambuzi wa washtakiwa kutambuliwa eneo la tukio inaonesha wazi walikuwa na nia ya kujaribu kupora takribani Sh 150 milioni mali ya benki ya NMB zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro tawi la Wami.” Anasema Jaji Rugazia.


Anasema siku hiyo ya huzuni ya Aprili 20,2006 majambazi hao walilivamia gari hilo kwa lengo la kupora lakini bila ya kuwa na huruma yoyote walilimiminia risasi na kuwaua D 6866 Konstebo Abdallah Marwa na mfanyakazi wa NMB tawi la Wami Morogoro, Ernest Manyonyi.


Walifanya tukio hilo nyakati za saa 6:30 mchana, eneo la Ubungo Mataa jijini Dar es Salaam kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma.


Akiendelea kusoma hukumu hiyo, Jaji Rugazia aliwaachia huru washtakiwa Rashid Lemblisi, Philipo Mushi, Yassin Juma,


Hamisi Daud, MT 77754 Nazareth Amurike, MT 76162 Emmanuel Lameck, James Chamangwana na Hussein Idd baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi hiyo.


Kwa upande wa washtakiwa, Jackson Issawangu aliyekuwa mshtakiwa wa sita katika kesi hiyo na Mussa Mustafa aliyekuwa mshtakiwa wa 10 waliachiwa huru awali baada ya mahakama hiyo kuwaona kuwa hawana kesi ya kujibu.


Hadi wanaachiwa huru jana, washtakiwa hao walikuwa wamekwisha kaa rumande kwa muda wa zaidi ya miaka 8. Kwa habari zaidi Usiache kusoma gazeti lako la Mwananchi leo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: