BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWIMBAJI MAARUFU NYIMBO ZA INJILI TANZANIA, FLORA MBASHA AENDA MAHAKAMANI KUDAI TALAKA ILI AACHIKE.


Flora mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha enzi za furaha ya ndoa.


Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania, Flora Mbasha, amekwenda katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar-Es-Salaam, akiomba kuvunjwa kwa ndoa yake na mumewe Emanuel Mbasha.

Flora amefungua kesi ya madai namba 64 ya mwaka huu kesi ambayo inasikilizwa na hakimu mkazi,Devota Kisoka.

Flora anadai kuomba kuvunja ndoa hiyo na apewe talaka ni kutokana na tabia ya mumewe kumpiga,kumnyanyasa na kushindwa kumpatia matibabu.
http://api.ning.com/files/vKR8mtf*1crw3iaIkV4YG5M*rvBuJCnjM0ls*2WqNKISmobKyuFNp-fhpiSMkDk17Pwb-2tjb9lbeBxy5yXg9ocJbocD2RQu/mbashakeki1.jpgKatika hati hiyo ya madaianaendelea kudai kwamba mgogoro wao waliwahi kuufikisha kwa ustawi wa jamii,kwa ajili ya upatanishi lakini ilishindikana wakashauriwa walifikishe suala lao mahakamani.

Flora anaiomba mahakama itoe talaka,iamuru aendelee kukaa na mtoto,matunzo ya mtoto yatoke kwa mbasha na wagawane mali walizochuma pamoja.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: