BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDANDA FC KUKIPIMA KIKOSI CHA FRIENDS RANGERA MAANDALIZI LIGI DARAJA LA KWANZA MZUNGUKO WA PILI DHIDI YA LIPULI.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjBeICqn1h2nqsGfPupDeVLw-UtuxWCfZaHTqYfYpyqLSLQWAzgMTGsCcfQmalhKp9tGKEYC_Mq-tfnp7tgA97lUpgoOzy-_7Ei1hfdF0UE-OWbskNOwuGETAJdumWuEKGuue_hoOAZ7Yc/s1600/FRIENDS+RANGERS+KIKOSI.jpg
KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, kesho kinajitupa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni Mwembechai, kuvaana na timu ya Ndanda FC ya Mtwara, katika mchezo wa kirafiki wa kijaindaa na mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza.

Ofisa habari wa timu hiyo Asha Kigundula, alisema kikosi hicho kinashuka dimbani kikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo inayoanza kutimua vumbi Ijumaa ya Desemba 26.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa michuano hiyo ambapo wao wataanzia ugenini dhidi ya Lipuli ya Iringa, imejipanga kupata mechi kadhaa za kirafiki, ambapo kesho Jumapili itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Ruvu Shooting.

Kigundula alisema kuwa kikosi chao kipo katika maandalizi makali ya kuhakikisha kinaendeleza rekodi yake ya kutofungwa kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo.

Alisema timu yao chini ya kocha wake Ally Yusuph 'Tigana' kimewasajili Haruna Moshi 'Boban' Amir Maftah, na Robert, wengine ambao wamekuja kwa mkopoWine Abbas kutoka Ruvu Shooting na Mahamod Osman kutoka Coastal Union.

"Tunaendelea kukinoa kikosi chetu kwa kupata mechi nyingi za kirafiki lengo letu ni kuendelea na safari yetu ya kupanda daraja, ambapo msimu ujao tunataka kucheza ligi kuu"alisema Kigundula.

Friends Rangers inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi daraja la kwanza, huku Majimaji ikishika usukani wa ligi hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: