BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SPIKA WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI MARGARET ZZIWA AVULIWA USPIKA NA WABUNGE 39.

http://www.makuruki.com/local/cache-vignettes/L643xH429/zziwa-2-3b98b.jpgSpika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Margaret Zziwa. 


SPIKA wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Margaret Zziwa hatimaye ameng’olewa na baadhi ya Wabunge wa Bunge hilo.

Wabunge hao walipiga kura jana huku Ofisi ya Bunge hilo ikitoa saa 48 kwa wabunge wa Bunge la Uganda kupeleka majina yao ili uchaguzi wa Spika mwingine kutoka nchi hiyo uweze kufanyika.

Kura hizo zilipigwa jana mchana na kutangazwa na Kaimu Spika kutoka nchini Uganda, Chris Ukomu ambaye ndiye alikuwa akiendesha kikao hicho.

Baadhi ya wabunge kutoka nchi mbalimbali, waliochoshwa na utendaji wa spika huyo walipiga kura na kusikiliza maazimio ya Kamati ya Sheria, Kanuni na taratibu. Idadi ya wabunge waliokuwepo ndani ya Bunge hilo ilikuwa ni 39.

Waliopiga kura za ‘Ndio’ kwa ajili ya kumng’oa Spika huyo ni 36 huku kura mbili zikisema ‘Hapana’.

Kura moja iliharibika. Awali, kabla ya upigaji kura huo, ambao uliongozwa na Okomu, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Kanuni na Taratibu, Frederic Ngenzebuhora alisoma tuhuma mbalimbali zinazomhusu spika huyo, ikiwemo kutoendesha ofisi hiyo kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria.

Alisema kutokana na madai mbalimbali, kamati hiyo imeona Spika huyo ni mtu anayejali maslahi yake badala ya maslahi ya wanajumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo wameona ni heri akae pembeni ili achaguliwe Spika mwingine kutoka Uganda.

Akifafanua tuhuma mbalimbali dhidi ya Spika huyo, Ngenzebuhora alisema Kamati ilipata ushahidi wa mkanda wa video ukimwonyesha mume wa Spika, Fransic Babu akijaribu kuingia kwenye chumba cha wageni maalum (VIP), ambapo Mwenyekiti wa Marais wa EAC (hawakumtaja jina) alikuwa akifanya kikao cha faragha na wenyeviti wa EALA kutoka nchi wanachama wa EAC.

Video hiyo ilimwonyesha Babu akiwatukana wabunge hao na kuwashutumu kwa kutaka kumng’oa mkewe madarakani pia Spika katika barua yake ya Januari 28, 2013 kwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa EAC, alitoa taarifa ambayo si sahihi.

Madai mengine ni Spika huyo analipwa dola za Marekani 3,000 kwa mwezi kwa ajili ya nyumba na pia halipwi posho ya kujikimu wakati wa mikutano ya EALA nje ya Arusha. 


Pia, Spika huyo anawabeba baadhi ya wabunge wa Bunge hilo na kuwapa safari za vikao nje ya nchi zaidi ya mara tatu huku wabunge wengine wakisafiri mara chacheHABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: