BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA TUKIO LA AJALI ILIYOHUSISHA GARI LA MEYA MANISPAA YA MORO NA BASI LA HAPPY AFRIKA NA KUJERUHI WAANDISHI WAWILI, MEYA NA DEREVA WAKE MOROGORO.

 http://jumamtanda.blogspot.com/
Mwandishi mpiga picha wa ITV, Hussein Nuha (30) akiwa katika wodi ya daraja la kwanza akiugulia maumizi baada ya kupata ajali eneo la barabara kuu ya Dar es Salaam kwa kuligonga basi la Happy Afrika lililokuwa likitokea Njimbe kwenda Dar es Salaam baada ya kuingilia msafara wa mkuu wa mkoa wa Morogoro na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kabla ya kuhamishiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi kwa upande wa kichwa jana.PICHA/MTANDA BLOG.

Mwandishi wa gazeti la Mtanzania mkoa wa Morogoro, Kuty Libenanga kulia akisaidia huduma ya kwanza kwa mwandishi mpiga picha wa ITV, Hussein Nuha wakati akifikishwa hospitalini hapo.

Mwandishi na mpiga picha wa StarTV Morogoro, Jackson Monela na Kuty Libenanga wakimwangalia Hussein Nuha baada ya kupatiwa huduma ya kwanza.
http://jumamtanda.blogspot.com/
MEYA WA MANISPAA YA MOROGORO:
Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Juma Nondo akiwa katika wodi ya daraja la kwanza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya kupata ajali na waandishi wawili na dereva wake ambapo walijeruhiwa vibaya.
Meya wa Manispaa ya Morogoro akiwaonyesha ndugu wa karibu sehemu ya mchubuko katika mguu baada ya kupata ajali hiyo.
 Baadhi ya madiwani wakimsaidia Meya huyo.
Meya akipelekwa katika chumba cha kupiga picha ya X-RAY kwa ajili ya uchunguzi wa mkono wa kushoto ambao alikuwa akilalamika maumivu ambapo baada ya uchunguzi huo umebainika kuvunjika.http://jumamtanda.blogspot.com/Mwandishi mpiga picha wa TBC 1, Anita Chali naye akiwa katika hospitali hiyo baada ya kupata ajali.

Dereva wa gari la Meya wa Manispaa ya Morogoro, Ally Mwambara akiwa katika kitanda cha wagonjwa akielekea wodini kulazwa baada ya kupata ajali eneo la Mizambarauni kwa kugongana na basi la Happy Africa lililokuwa likitokea Njombe kuelekea Dar es Salaam katika barabara kuu ya Dar es Salaam-Morogoro wakati wakitoka katika ziara ya mkuu wa mkoa wa Morogoro jana.
 Gari lililopata ajali na kujeruhi watu wanne.
Basi la Happy Afrika likiwa linaonekana sehemu maalum ya kuwekea mizigo ikiwa imeharibika baada ya ajali hiyo eneo la tukio.

Na Lilian Lucas, Morogoro.
Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutengwe umepata ajali jana saa 9.30 alasiri eneo la Mizambarauni Darajani barabara kuu ya Dar es Salaam-Morogoro.


Katika ajali hiyo, Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Juma Nondo amevunjika mkono wa kushoto, pamoja na waandishi na wapigapicha wawili wa Kituo cha ITV, Hussein Nua na Anitha Chali wa Televisheni ya Taifa (TBC) pamoja na dereva wa meya huyo, Ally Mwambara wamejeruhiwa vibaya.


Basi la abiria la Happy Afrika aina ya scania lililokuwa likitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam linadaiwa lilitaka kulipita gari lililokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara ndipo lilipoligonga gari hilo la Manispaa ya Morogoro aina ya Nissan Patrol.


Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Meya Nondo alisema wakiwa katika gari lao, aliliona basi likija kwa kasi sana na kutaka kukatiza na kwenda upande wa kulia bila kuangalia mbele ndipo wakagongwa.


“Yule mwenye basi alikuwa anaendesha kwa kasi sana akawa anakuja kwenye gari letu kwa kutaka kukatiza upande wa pili na sisi tukapigwa ubavuni, ndicho nilichokiona,” alisema Nondo.


Msafara huo wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ulikuwa katika ziara tangu asubuhi kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na wakiwa wanakwenda kupata chakula cha mchana ndipo ajali ilipotokea.


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Godfrey Mtei alithibitisha kupokea majeruhi wanne na kwamba wanapatiwa matibabu na majeruhi wawili hali zao ni mbaya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: