BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAWA NDIYO WABUNGE WATANO WALIOITISHA SERIKALI KATIKA BUNGE LA 19, CHADEMA YAFUNIKA MJINI DODOMA.

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2329950/highRes/754223/-/maxw/600/-/kfriei/-/lugola.png 

Mbunge Kangi Lugola (Mwibara - CCM.

Dodoma.
Wabunge watano wamelitikisa Bunge tangu mkutano wa 19 wa Bunge ulipoanza kutokana na michango yao binafsi katika mijadala ya miswada ya sheria mbalimbali iliyowasilishwa bungeni.



Tathmini iliyofanywa na gazeti hili tangu kuanza kwa vikao hivyo, imeonyesha wabunge hao ndio waliokuwa wakisimama mara kwa mara kuchangia hoja.


Hoja zilizozungumzwa na wabunge hao kwa nyakati tofauti ziliitikisa Serikali na kusababisha aliyekuwa akikaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni, Profesa Mark Mwandosya, kiti cha Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju kusimama kutoa ufafanuzi.


Waliotikisa
Wabunge waliotikisa Serikali katika michango yao ni Kangi Lugola (Mwibara - CCM), Tundu Lissu (Singida Mashariki - Chadema), John Mnyika (Ubungo-Chadema), Chrisowaja Mtinda (Viti Maalumu-Chadema) na Habib Mnyaa (Mkanyageni-CUF).


Lissu
Machi 20 mwaka huu wakati akichangia muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa, aliibana Serikali huku akitumia dakika 125 kupinga muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha vipengele.


Mara kadhaa Masaju, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), Jenister Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu walisimama kumwelewesha mbunge huyo, lakini alishikilia msimamo wake, huku akisema muswada huo una mgongano wa kisheria kuhusu mamlaka ya kuweka utaratibu wa kutangaza maafa na kutangaza hali ya hatari, akisema kuwa sheria hiyo imempora Rais madaraka ya kutangaza maafa na kuyapeleka kwa waziri.


Mnyika
Aliibuka Machi 26 wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha Muswada wa Takwimu wa mwaka 2013, kuibuka na hoja ambayo lilikuwa halifahamiki kwamba katika muswada huo kuna kipengele kinachotoa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini isiyopungua Sh10 milioni kwa mtu au chombo cha habari kitakachofanya makosa ya kutoa takwimu zisizokuwa sahihi.


Mbunge huyo akihoji sababu za kutobadilishwa kwa vipengele vya muswada huo vyenye utata kama ambavyo Serikali iliahidi Novemba mwaka jana baada ya muswada huo kukwama kupitishwa kutokana na wabunge wengi kupinga vipengele vyenye utata, kikiwamo kipengele hicho.


Mnyaa
Mbunge huyo wa Mkanyageni aliibuka Machi 20 na kutoa hoja ya kutaka muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji namba 54 wa mwaka 2014, kutojadiliwa bungeni kwa sababu unagusa mambo ya muungano, ambapo katika hoja yake alisema kama uhamiaji ni eneo la muungano, iweje muswada huo upitishwe na Bunge hilo bila theluthi mbili ya wabunge kutoka Zanzibar kama Katiba inavyotamka.


Mvutano huo ulisababisha Masaju kufafanua kuwa kati ya masuala yanayogusa muungano, ambayo yakifanyiwa marekebisho yanahitaji kupitishwa na theluthi mbili za wabunge wote wa Tanzania Bara na visiwani, uhamiaji na masuala ya silaha hayamo.


Licha ya ufafanuzi huo, Spika wa Bunge Anne Makinda aliahirisha kujadiliwa kwa muswada huo pamoja na mingine miwili ya takwimu na usimamizi wa kodi ili kupata nafasi nzuri ya kupitia vifungu vya sheria kuona kama jambo hilo ni sahihi ama la.


Lugola
Machi 24 wakati akichangia muswada wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya, alizua taharuki baada ya kueleza kuwa amekwama kuwataja vigogo wanaojihusisha na uuzaji wa dawa hizo kwa kuhofia usalama wake.


Mtinda
Mbunge huyo aliliteka Bunge Machi 23 wakati akichangia mjadala wa muswada wa Sheria ya Mifumo ya Malipo baada ya kuzilipua kampuni za simu na benki kuwa zinawaibia Watanzania na hakuna sheria ya kuzishitaki. Hata hivyo, hoja zake zilijibiwa na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: