BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAPT JOHN KOMBA AKWAMISHA KESI YA HALIMA MDEE KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU DAR ES SALAAM.


Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (pichani), baada ya mbunge huyo kuteuliwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, marehemu Kapteni John Komba.

Mdee na wenzake, wanakabiliwa na mashitaka ya kupinga amri halali ya Jeshi la Polisi na kukusanyika isivyo halali kwa lengo la kwenda Ikulu.

Kesi hiyo iliahirishwa jana na Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda.

Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki, alidai kuwa upande wa Jamhuri ulikuwa na shahidi mmoja lakini waliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza kwa sababu mshtakiwa wa kwanza hayupo na ushahidi unamzungumzia yeye.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala, alipinga maombi hayo kwamba ushahidi uendelee kusikilizwa.

Upande wa Jamhuri ulidai kesi hiyo haiwezi kuendelea kusikilizwa mpaka mshtakiwa atakapomaliza udhuru wake.

Mbali na Mdee, washtakiwa wengine ni Rose Moshi, Renina Peter maarufu kama Lufyagila, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fangel, Edward Julius, Martha Mtiko na Beatu Mmari.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa Oktoba 4, mwaka 2014, katika mtaa wa Ufipa, jijini Dar es Salaam, walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi Emmanuel Tille, kwa niaba ya Jeshi la Polisi.

Pia wanadaiwa siku hiyo walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kutembea kwenda Ofisi ya Rais.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: