BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SAFARI YA MWISHO YA KAPT JOHN KOMBA, DK KIKWETE AONGOZA MAMIA KUMZIKA MAZISHI YAKE MKOANI RUVUMA.


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa, Mkoani Ruvuma.

Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbinga Mhashamu John Ndimbo akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma jana.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa, Mkoani Ruvuma. (Picha na Freddy Maro)

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana, Sixtus Mapunda pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali yaTanzania kwenda kumzika marehemu Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.


Mke wa Marehemu Kapteni John Komba, Salome (kushoto) akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu.

Watoto wa marehemu Kapteni John Komba wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba yao.

Watoto wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yao .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyezikwa kwenye makaburi ya kijiji cha Lituhi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Damian Komba aliyezikwa kijijini kwake Lituhi.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Lameck Mchemba pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyefariki jijini Dar es Salaam tarehe 28 februari na kuzikwa kijijini kwake Lituhi tarehe 3 Machi 2015.


Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu (kulia) akiweka shada la maua pamoja na mkewe kwenye kaburi la Kapteni John Komba. Msanii nguli Khadija Kopa akiwa katika huzuni kubwa mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.











































(Picha kwa Hisani ya Kamanda wa Matukio bloggs)

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: