BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SAKATA LA KUWANIA URAIS KWA LOWASSA: MASHEIKHE WA BAGAMOYO WAKANUSHA, WAO SIYO FEKI, BAKWATA INAWATAMBUA !!.


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.


Masheikh 50, kutoka Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani, waliokwenda Mkoani Dodoma kwa ajili ya kumshawishi Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kugombea urais, wamesema wao ni masheikh halali na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) linawatambua.


Akizungumza kwa niaba ya wenzake mjini Bagamoyo jana, msemaji mkuu wa masheikh hao, Alhaji Hassan Kilemba, alielezea kusikitishwa na tamko la kuwakana ambalo lilotolewa na Sheikh Mkuu wa Bagamoyo Abdulkadir Ramiya.

Alisema tamko hilo limewasikitisha kwa sababu limesababisha watafsiriwe na jamii kama masheikh ‘feki’ na wakati wanatambuliwa Bakwata.

Licha ya kukiri wazi kuwa safari yao haikuwa na msukumo wowote wa Bakwata Wilaya ya Bagamoyo, lakini Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ambaye pia ni Sheikh wa Tarikatul Kadirya aliitambua safari yao kwa sababu alipewa taarifa kabla.

“Tunasikitishwa na kauli ya sheikh mkuu kusema haitambui safari yetu ya kwenda Dodoma wakati tulimtaarifu kabla na akatukubalia…ametugeuka baada ya vigogo wa CCM kumfuata,” alisema Sheikh Kilemba.

Katika kudhihirisha kuwa Bakwata inawatambua masheikh hao, Sheikh Kilemba alisema wakati wakiwa safarini ulifanyika uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi wa Bakwata wilayani hapo ambapo wajumbe wawili waliokuwamo kwenye msafara huo majina yao yalipita katika uchaguzi huo.

Naye Sheikh Sharifu Muhidin Mapanga, alisema kuwa amesikitishwa kuambiwa kuwa yeye ni Sheikh ‘feki’ na wakati nafasi yake ni zaidi ya Sheikh.

Aliongeza kuwa safari yao ya kwenda Dodoma haikuwa na ushawishi wowote wa pesa bali walifanya hivyo kwa mapenzi ya mioyo yao kwa sababu ya wanatambua utendaji kazi wa Lowassa.

“Anayekubalika na wengi ni wa Mungu kwa hiyo kutambua tumempa baraka zote hata kama litatokea lolote ataendelea kuwa na baraka zao,” alisema.

Alipotafutwa Sheihk Mkuu wa Bagamoyo, Abdulkadir Ramiya ili atoe ufafanuzi wa madai hayo simu yake ya kiganjani haikupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi akujibu.

Sheikh mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Abdulkadir Ramiya alikaririwa na vyombo vya habari akiwaasa waislamu kufuata misingi ya kidini na kuacha kutumiwa. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: