BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TIMU YA SOKA YA MWANANCHI FC KUSAKA UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI KOMBE LA STANDARD CHARTERED KENYA.


Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi(kushoto) akimkabidhi Bendera ya Taifa, nahodha wa timu ya Mwananchi FC, Majuto Omar, kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Standard Chartered Afrika Mashariki yatakayofanyika Kenya Jumamosi. Wa pili kushoto ni Ofisa Mtenda Mkuu wa Benki ya Standard Charterd, Liz Lloyd. Kulia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Bakari Machumu. Picha na Venance Nestory.


Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ameikabidhi bendera ya Taifa, timu ya Soka ya Kampuni ya Mwananchi Commnications Limited (Mwananchi FC), na kuitaka ipambane kikamilifu na kuhakikisha inatwaa ubingwa wa Afrika Mashariki kwenye Michuano ya Kombe la Standard Chartered.


Mwananchi FC inayoondoka nchini leo kwa ndege ya Shirika la Kenya (KQ ) itaiwakilisha nchi kwenye mashindano hayo yanayofanyika kesho jijini Nairobi.


Katika hafla hiyo, Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu alisema timu hiyo imefanya mazoezi ya kutosha na wanaamini hawataishia Nairobi, bali watafuzu kuiwakilisha Afrika Mashariki katika mashindano ya dunia baadaye mwezi huu jijini Liverpool.


“Kampuni tuliiunga mkono timu yetu kwa kuhakikisha inafanya vizuri na hatimaye kutwaa ubingwa wa Taifa na kufuzu kuiwakilisha nchi. Japo ushindani ulikuwa mkubwa, tunaiamini timu yetu na tunaamini itafanya vizuri na kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki. Pia, niipongeze Benki ya Standard Chartered kwa kuandaa mashindano haya,” alisema Machumu.


Malinzi aliiahidi timu hiyo kuwa, ataipokea Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam na kuisindikiza hadi makao makuu ya kampuni hiyo, Tabata Relini, endapo itarejea na ubingwa.


Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Liz Lloyd alisema mshindi kwenye mechi ya Jumamosi atakata tiketi ya moja kwa moja kuiwakilisha Afrika Mashariki kuwania Kombe la Standard Chartered kwenye Uwanja wa Anfield, England.


Liz alisema kwenye mashindano ya dunia kutakuwa na timu za Afrika Magharibi, Afrika Kusini, China na nchi nyingine za Ulaya.


Nahodha wa Mwananchi FC, Majuto Omary alisema wamejiandaa vizuri na kuahidi kurejea na ubingwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: