BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

YANGA SC YATWAA UBINGWA LIGI TANZANIA BARA MBELE YA POLISI MORO SC KWA KUILAZA BAO 4-1 UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM.


Washambuliaji wa Yanga SC, Amisi Tambwe na Simon Msuva wakishangilia moja ya mabao yao 4 dhidi ya Polisi Moro SC katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo, ambapo tayari Yanga wametwaa ubingwa wa ligi kuu ikiwavua rasmi Azam FC.


Dakika ya 38 Polisi Moro wamepata bao la kujifutia machozi baada ya shuti la mbali lililofumuliwa na mshambuliaji Bantu Admini na kufanya matokeo kuwa Yanga SC 4-1 Polisi Moro SC baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mchezo huo mbao Yanga SC wametawazwa mabingwa wapya kufuatia kumvua rasmi bingwa mtetezi Azam FC.


Dakika ya 21 kipicha cha pili Simon Msuva anaipatia Yanga SC bao la nne na kuifanya Yanga SC iendelee kuongoza kwa bao 4-0 dhidi ya Polisi Moro SC katika mchezo unaochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Dakika ya saba kipindi cha pili mshambuliaji Amis Tambwe anaipatia Yanga SC bao la pili baada ya kazi nzuri ya Simon Msuva jygongea vyema na kiungo Harouna Niyonzima kabla ya Msuva kufumua shuti kali akiwa ndani ya 18 na mlinda mlango wa Polisi Moro SC, Abdu Badi kuutema kisha Tambwe kumalizia mpira huo wavuni, Yanga SC 2-0 Polisi Moro SC.

Dakika ya 15 kipindi cha pili, Amis Tambwe anapachika bao la tatu baada ya kazi nzuri ya Mrisho Ngassa na kuifanya Yanga iongoze kwa bao 3-0 yote yakipachikwa na Amis Tambwe.

Mshambuliaji Yanga SC, Amis Tambwe amepachika bao la kuongoza dakika ya 42 na kuiwezesha timu yake kwenda mapumziko kutoka kifua mbele kwa kuongoza bao hilo dhidi ya Polisi Moro SC katika mchezo unaofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: