BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KLABU YA MBEYA CITY YAMKATIA RIFAA JUMA NYOSO IKIPINGA ADABU YA KUFUNGIWA MIAKA MIWILI LIGI KUU TANZANIA BARA.


Juma Nyosso 


Dar es Salaam. Suala la kufungiwa nahodha wa Mbeya City, Juma Nyoso limechukua sura mpya baada ya klabu hiyo kuwasilisha nia ya kukata rufaa.


Jana, klabu hiyo ilieleza kuwa itawasilisha rufaa hiyo leo kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi (TPLB) ikipinga adhabu hiyo ya miaka miwili na faini ya Sh2 milioni.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mussa Mapunda alisema jana kuwa taratibu za rufaa hiyo zilikuwa zikiendelea pamoja na kukusanya ushahidi, ukiwamo wa mikanda ya video ya mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi wiki iliyopita.

Alisema wamebaini kuwa mchezaji wao (Nyoso) alihukumiwa bila kusikilizwa, pia wachezaji wa Azam, akiwamo John Bocco Adebayor waliohusika katika tukio hilo wakiachwa bila kuchukuliwa hatua. Wakati hayo yakiendelea, TPLB imesema timu hiyo inayo haki ya msingi kukata rufaa kupinga hukumu hiyo aliyopewa nahodha wao.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura alisema jana kuwa adhabu ya Nyoso iko pale pale na endapo klabu yake haikuridhishwa na hukumu hiyo. ina haki ya kukata rufaa.

Alisema kamati yao ilichukua hatua ya kumfungia Nyoso kwa miaka miwili kwa kile ilichoeleza ni kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.

“Adhabu ya Nyoso iko pale pale na endapo Mbeya City wataona mchezaji wao hajatendewa haki, milango hiko wazi kukata rufaa,” alisema Wambura.

Naye katibu mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa alisema jana kuwa Mbeya City ina haki ya kukata rufaa, na wao wataipitia rufaa hiyo kuona yaliyomo na kama yana mantiki yatashughulikiwa na kamati husika.

“Tutapitia rufaa yao, tuone wamelalamikia au kupinga nini, tutawasilisha kwenye kamati husika kwa hatua zinazofuata,” alisema Mwesigwa jana alipoulizwa kuhusu dhamira ya klabu hiyo kupinga adhabu hiyo.

Juzi, Nyoso alitoka hadharani na kueleza kuwa amefungiwa bila kupewa haki ya kusikilizwa, hakuwa na dhamira ya kutenda kosa analotuhumiwa kulitenda.

Kamati ya uendeshaji wa Ligi Kuu ilimfungia Nyoso kucheza soka kwa miaka miwili na faini ya Sh 2 milioni kufuatia kitendo cha udhalilishaji alichodaiwa kumfanyia mchezaji wa Azam, John Bocco katika mchezo uliozikutanisha timu hizo na Azam kushinda mabao 2-1.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: