BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VYAMA VYA UPINZANI VYABANWA MBAVU NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI BAADA YA KUVUNJA SHERIA YA UCHAGUZI MKUU 2015.

 
Moshi. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa muda wa saa 48 kwa vyama vya siasa vilivyobandika picha za wagombea maeneo yasiyostahili Jimbo la Moshi mjini kuyaondoa mara moja.

Agizo hilo lilitolewa jana na mwenyekiti wa kamati ya maadili ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Shaban Ntarambe ambaye alisema hadi kufikia kesho ziwe zimeondolewa.

Hata hivyo Agizo hilo litaviathiri zaidi vyama vya upinzani kutokana na mabango mengi ya wagombea wao kubandikwa sehemu zisizostahili ukilinganisha na ya mgombea ubunge wa CCM, Davis Mosha.

Wakati picha za wagombea wengi wa upinzani zikiwa zimebandikwa hadi kwenye milingoti ya umeme na simu, picha za Mosha zimebandikwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya matangazo ya biashara.

Sambamba na wagombea ubunge wa vyama vya upinzani, lakini kwa sehemu kubwa picha za wagombea Udiwani katika kata mbalimbali, baadhi yake zimebandikwa maeneo yasiyostahili.

Agizo la kuondoa mabango na vipeperushi maeneo yasiyoruhusiwa limetolewa na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Shaban Ntarambe katika barua aliyowatumia makatibu wa vyama vya siasa.

Katika barua yake ya Oktoba 2, yenye kumb MMC/A.40/48/Vol.XXV/117, Ntarambe kwenda kwa makatibu wa vyama vya siasa, agizo lake linatokana na maazimio ya kamati hiyo ya Septemba 30.

Kufuatia agizo hilo, Kaimu Katibu mwenezi wa Chadema katika jimbo hilo, Mohamed Ally alisema agizo hilo linalenga kuvikandamiza vyama vya upinzania ambavyo havina uwezo kununua maeneo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: