BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KASI YA UTENDAJI KAZI YA RAIS MAGUFULI YAMTIA UOGA KATIBU MKUU WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI.

RAIS WA TANZANIA DK JOHN MAGUFULI

Kibaha. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Yohana Budeba amewataka wadau na wanaharakati wa kilimo na mazingira kushirikiana na wizara yake kubainisha fursa za maendeleo ili kuendana na kasi ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.

Alitoa wito huo mjini hapa jana, alipokutana na viongozi wa Chama cha Wanawake Wataalamu wa Kilimo (Tawlae) na Jukwaa Huru la Wadau wa Kilimo (Ansaf) wanaojadiliana juu ya changamoto na fursa za kilimo bunifu kwa usalama wa chakula na lishe.

Akifungua mkutano huo wa siku tatu, Dk Budeba alisema zipo fursa nyingi katika kilimo, ufugaji na uvuvi ambazo zikitumika ipasavyo, zitapunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini.


 “Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la Kumi na Moja, Rais Magufuli aliipa kipaumbele wizara yangu. Hivyo, natoa wito kwa kila mwenye mchango wa kusaidia ubunifu katika sekta ya kilimo ili kuwanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Teknolojia na ubunifu wa kisayansi ni miongoni mwa vitu vinavyokosekana kwa wakulima wetu nchini,” alisema katibu huyo.

Washiriki wa mkutano huo walisema wanatarajia kupata majibu ya maswali yatakayoisaidia wizara hiyo kutunga sheria, sera na kanuni zitakazokuwa na manufaa kwa wadau wa kilimo.

Mwenyekiti wa Tawlae, Dk Sophia Mtole, alisema kitu kikubwa wanachokiangalia ni namna wakulima watakavyonufaika na kazi zao za mikono walizowekeza shambani kwa kuongeza uzalishaji wa mazao.

“Tumeamua kuwa sehemu ya kutafuta suluhu kwa kero zilizopo na mpaka mwisho wa semina hii tutakuwa na mapendekezo muhimu kwa Serikali,” alisema Dk Mtole.

Mkurugenzi Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge, alisema kuna fursa nyingi ambazo wakulima wanapaswa kuzifahamu ili wanufaike.CHANZO:MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: