BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS DK JOHN MAGUFULI NA WAZIRI MKUU WAKE MAJALIWA KASSIM WAWAHENYESHA VIONGOZI WAANDAMIZI WA MAMLAKA YA BANDARI (TRA) BAADA YA UPOTEVU WA MABILIONI YA FEDHA DAR ES SALAAM

RAIS MAGUFULI AMSIMAISHA KAZI KAMISHA MKUU WA TRA.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia leo Novemba 27/ 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema leo asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam.

Hatua hiyo imekuja baada ya kubaini kupitishwa kwa makontena zaidi ya 300 na kusababishia hasara Serikali ya zaidi ya shilingi bilioni 80.

Rais Magufuli pia amemteua Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo mpaka hapo uchuguzi utakapo kamilika.

Taarifa hiyo iliyosomwa na Katibu Mkuu Kingozi, Balozi Ombeni Sefue Ikulu jijini Dar es salaam, imewataka maofisa wote wa TRA kutosafiri nje ya nchi mpaka pale uchunguzi dhidi yao utakapo kamilika. 


WAZIRI MKUU AIBUA MADUDU YA UPOTEVU WA MAKOTENA 346 YENYE DHAMANI YA SH 80 BILIONI BANDARINI YA DAR ES SALAAM.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.


Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia.


Maafisa hao, ambao kwa sasa tunahifadhi majina ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.


Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya Sh 80 Bilioni ambayo kumbukumbu za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA kutoonekana.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo.


Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa TRA na TPA.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: