BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU 14 WA CCM WANUSURIKA KIFO BAADA YA NYUMBA SITA KUCHOMWA MOTO USIKU WA MANENO KIJIJI CHA IPUTI ULANGA.

Mbunge Mteule jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga kushoto akizungumza jambo na Ibrahim Mkingi (22) baada ya tukio la nyumba sita za wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) kuchomwa moto usiku wa saa 8 Novemba 22 mwaka huu katika kijiji cha Iputi kata ya Mbunga tarafa ya Mwaya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro. PICHA/JUMA MTANDA, MOROGORO 

Na Juma Mtanda, Mwananchi. Zaidi ya watu 14 wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa chama cha mapinduzi (CCM) wa kijiji cha Iputi kata ya Mbunga tarafa ya Mwaya wilaya ya Ulanga wamenusurika kifo baada ya nyumba zao kuchomwa moto usiku wa Novemba 24 mwaka huu.

Kutokana na kuchomwa moto nyumba hizo jeshi la polisi mkoani Morogoro likiwashikilia watu watano wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo, huku likiendelea kuwatafuta watu wengine ambao idadi yao haijafahamika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alilieleza gazeti hili kuwa nyumba sita zimechomwa moto katika kijiji cha Iputi kata ya Mbuga tarafa ya Mwaya Nombea 24 majira ya saa 8 usiku huku watuhumiwa zaidi ya watano wakikamatwa na kuhojiwa.

“Watuhumiwa watano wamekamatwa na kuhojiwa lakini wengine wamekimbia, lakini tayari nimemtuma mkuu wa upelelezi makasa ya jinai mkoa wa Morogoro kuhakikisha watuhumiwa wengine wanapatikana na kufikishwa mahakamani muda wowote baada ya upelelezi kukamilika,”.alisema Paulo

Paulo alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa tukio hilo linahusishwa na itikadi za kisiasa kati ya vyama vya siasa vya chama cha mapinduzi (CCM) na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Baadhi ya wananchi wakizungumza mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Ulanga na Mbunge Mteule wa jimbo hilo Goodluck Mlinga kijijini hapo juzi, ambao wengine ni wanachana wa CCM na walionusurika na kifo, walieleza kuwa tukio hilo lilitokea majira saa 8 usiku kwa nyumba hizo kuchomwa moto na watu wanaodhani kuwa ni Cahdema
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Christina Mndeme (wa pili kutoka kushotoi) akizungumza jambo wakati kamati yake ilipotembelea watu wa chama cha Mapinduzi (CCM) kufuatia nyumba sita kuchomwa moto usiku wa manane Novemba 24 na watu wasiofahamika kijiji cha Iputi kata ya Mbuga tarafa ya Mwanya Ulanga mkoani Morogoro, wa kwanza kushoto ni Mbunge Mteule jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga na mmiliki wa nyumba hiyo, Rashidi Chikoko.PICHA/JUMA MTANDA, MOROGORO


Mmoja wa watu hao, Ibrahim Mkingi (22) alieleza kuwa majira ya saa 7 usiku alisikia sauti akiamshwa kutoka usingizini ya kumtaka afungue mlango na atoke nje ya nyumba huku akiona mwanga mkali wa moto na joto kabla ya kushuhudia nyumba yake ikiteketea kwa moto huo.

“Nilisikia sauti ya kuamshwa na kelele nyingi na baada ya kumka kutoka usingizi niliona mwanga wa moto na joto kali wakati watu mbalimbali wakifanya jitihada za kuniokoa maana kifo tayari kilikaribia endapo nisingeamshwa,”alisema Mkingi.

Mbunge Mteule wa jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga aliyefika kuwapa pole wahanga hao ameahidi kuzifanyia ukaratibi nyumba hizo ili zirejee katika hali yake na kuweza kutumika.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Christina Mndema, alieleza kusikitishwa na tukio hilo huku akiwataka wananchi kuwafichua wahalifu ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Mndeme alisema kuwa tukio hilo ni tukio la kiufalifu na uuaji jambo ambalo serikali haiwezi kuifumbia macho na  kuwahakikishia wananchi watu hao watasakwa kila kona ya wilaya hiyo.


“Hili tukio ni tukio la kinyama na uuaji lakini serikali haiwezi
kulifumbia macho, leo hii watu hawa wapo salama lakini tayari
wamepoteza mali ni miujiza ya mungu tu ndio iliyowaokoa na kifo watu hawa kwani waliochomewa nyumba moto wameingia katika
umasikini,”.alisema Mndeme.

Mkuu huyo aliwataka wananchi kutulia na kuendelea na maandalizi ya kilimo wakati serikali ikiendelea kutoa ulinzi eneo hilo na kuwasaka watu hao aliowaeleza kuwa wanafahamika.


Nyumba zilizochomwa moto na kuteketea kabisa ni pamoja na, Rashidi Chikolo na Ibrahim Mkingi wakati nyingine nne za Hassan Mkingi, Twaha Ngegame (33), Saidina Saidi Mfaume na Ramadhan Kalyahi zenyewe wananchi wakiwahi kuzima moto ili zisiteketee.

Uchunguzi wa awali uliofanywa na gazeti hili baada ya nyumba sita kuchomwa moto kijiji hapo umebaini kuwepo kwa uhasama baina ya vyama vya CCM na CHADEMA uliotokana na kutoridhwa kwa ushinda kiti cha udiwani kata ya Mbuga na uliowanya CCM iibuke kidedea kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Ulanga Novemba 22 mwaka huu.CHANZO:MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: