BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTANDA BLOG INAWATAKIA EID EL FITR MUBARAKA 2014

 
MTANDA BLOG inawatakia Waislamu wa Afrika Mashariki na ulimwenguni kote EID EL FITR MUBARAKA Njema na inawapongeza kwa kumaliza mfungo wa Ramadhani.
Tunamuomba Allah SW atukubalie ibada zetu za funga, kusoma Qur-ani, qiyamul-layli, swadaqa na amali nyengine pamoja na kuturuzuku fadhila zote za mwezi huo mtukufu na pia kutulipa lililobora zaidi ya hilo nalo ni radhi zake.

MTANDA BLOG inawakumbusha Waislam kutekeleza faradhi ya Zakatul-fitri na sunna zote za EID EL FITR kama ilivyotekelezwa katika Swala ya EID ikifuatiwa na kuvaa nguo mpya, kutembelea ndugu, jamaa na nyenginezo.

Pamoja na kuwa EID Ni furaha, MTANDA BLOG inawakumbusha Waislamu kuwa wao ni Ummah mmoja kote duniani na hivyo kuwataka wawafikirie Waislamu wenzetu ambao wanaingia katika EID hali ya kuwa wapo katika vita.

MTANDA BLOG inatoa shukurani za dhati wa wadu wote kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitr Mubaraka isherrhrkewe kwa amani na utulivu ili kudumisha upendo na mshikamano katika dunia hii. AMIN
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: