BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MCHEZAJI WA SOKA AFARIKI DUNIA WAKATI AKISHANGILIA BAO BAADA YA KUFUNGA LIGI YA INDIA. SAMBASOTI YASABABISHA KIFO KUFUATIA KUDONDOKA VIBAYA NA KUVUNJA MGONGO.

Yeşil sahada korkunç ölüm!
Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.

Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kwa timu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.

Ligi ya Mizoram ikimuombolea mchezaji Peter Biaksangzuala.



Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.

Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.

Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kupitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema : ''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka na mashabiki wa Mizoram. ''Peter Biaksangzuala

"Peter alikuwa mchezaji mzuri na mlinzi mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.''bbc
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: