BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MIMBA ZAONGEZEKA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA WAZIRI CELINA KOMBANI ULANGA.

http://lh5.ggpht.com/-DXTJcG9Gtp8/UpjLPIE8CjI/AAAAAAAAT64/ywRh56hFM1w/pregnant_thumb%25255B1%25255D.jpg?imgmax=800 
Wanafunzi 68 wa kike katika Shule ya Sekondari ya Celina Kombani, wameshindwa kuhitimu elimu ya kidato cha nne mwaka huu, kwa sababu mbalimbali zikiwemo mimba na utoro wa kudumu.


Hayo yalisemwa na Mkuu wa shule hiyo, Gabriel Munuo alipokuwa akizungumza katika mahafali ya pili ya kidato cha nne.


Alisema pamoja na mimba, kitendo cha baadhi ya wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha pili, pia kimechangia kuongeza idadi ya walioshindwa kuhitimu kidato cha nne.

“Wasichana wengi wameshindwa kuhitimu masomo yao kwa sababu ya kupata mimba na utoro uliokithiri. Mbaya zaidi ni kwamba baadhi ya wazazi wanashiriki kuficha maovu ya watoto wao,” alisema Munuo.

Kwa upande wao, wanafunzi wahitimu wamelalamikia upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi katika shule hiyo na kwamba tatizo hilo linasababisha wengi kufanya vibaya katika mitihani ya masomo hayo.


“Sisi tunamaliza, lakini ombi letu kubwa kwa mamlaka zinazohusika, ni kuangalia namna ya kumaliza tatizo la upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi, ili wenzetu wanaobaki wafanye vizuri katika masomo hayo,” ilisema sehemu ya risala ya wanafunzi hao.


Pia walizitaka mamlaka hizo, kuwachukulia hatua za kisheria, watu wanaowapa mimba wafunzi wa kike, ili kukomesha tatizo hilo.


Walisema hatua kama hizo, zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya wazazi wanaoshindwa kutoa ushirikiano wa kukamata na kuwafikisha mahakamani wanaume wanaowapa mimba watoto wao.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: