BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UKIFANYA UHALIFU, HII NDIYO NJIA YA KUKWEPA POLISI, UKIFAULU SAFI SANA LAKINI UKIBUGI KIDOGO TU IMEKULA KWAKO, AJIDAI MGONJWA MAHUTUTI KWA MIAKA MIWILI KUKWEPA MASHTAKA.

Alan Knighty alijidai kuwa mgonjwa mahututi ingawa alikamatwa na madaktari akiwa anajilisha

Mwanamume mmoja alitumia udanganyifu na kujidai kuwa mgonjwa mahututi kwa miaka miwili nchini Uingereza.


Alan Knight, mwenye umri wa miaka 47, kutoka mtaa wa Swansea, alimuibia mzee mmoja jirani yake pauni elfu arobaini kwa njia ya udanganyifu na kudai kuwa hangeweza kutembea kutokana na kupooza kutoka shingoni hadi miguuni.

Hii ilikuwa njama yake ili asiweze kukamatwa kwa kosa hilo. Inaarifiwa laikwepa polisi mara mbili kwani wakati hupo yeye mwenyewe alijipeleka hospitani ili asikamatwe na kushitakiwa. 

Knight na mkewe madukani
Kila wakati polisin walipotaka kumfikisha mahakamani , Knight alijipeleka hospitalini akidai kuwa hali yake imekuwa mbaya zaidi.

Hata hivyo siku zake za mwizi kushikwa zilifika pale wauguzi walipompata katika chumba chake hospitalini akiwa anakula , kupanguza mdomo wake na hata kuandika.

Kwa miaka miwili, Night alikwepa mkono wa sheria kwa kudai kuwa alikuwa hawezi kuamka wala kutembea na pia alikuwa tayari na uraibu wa kutumia gesi ya oxygen kama mtu ambaye hawezi kupumua bila usaidizi wa gesi hiyo.

Yote hayo yalikuwa uongo na ambayo yangewezekana tu kwa sinema. 

Hapa Knight alinaswa kwa kamera ya CCTV na polisi akiwa madukani

Alan Knight katika duka la Tesco, alinaswa na polisi kwa camera ya CCTV akisukuma gari la kubebea bidhaa ndani ya duka hilo wakati akidai kuwa mgonjwa mahututi.

Afisaa mmoja wa polisi Paul Harry, kutoka South Wales alisema: ‘Katika kazi yangu hii, sijawahi kuona kisa kama hicho ambacho kilipangwa na kutekelezwa kwa umaakini huo.'' 

Mkewe Knight ndiye alikuwa msaidizi wake katika sakata hii akimhudumia wakati wote

Mkewe mwanamume huyo mwenye watoto watatu , pia alikuwemo kwenye sakata kwani siku zote alionekane akimhudumia mumewe aliyejidai kuwa hali mahututi. T

Mbunge wa eneo la Swansea West aliambia BBC kuwa: "Nilikutana na Bi Hellen na akaniarifu ambavyo mumewe alikuwa na hali mbaya ya kiafya na kwamba walitendewa vibaya na polisi.''

Knight anakabiliwa na mashitaka 19 ikwemo wizi na ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: