BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UKWELI JUU YA WAZIRI WA ZAMANI KURUSHIANA RISASI NA MWANAYE WA KUMZAA MOROGORO SASA ZAWEKWA HADHARANI.


Kufuatia taarifa zilizozagaa mjini morogoro na kuripotiwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mbunge wa jimbo la morogoro kusini, Dk Lucy Nkya na mwanaye Jonas Nkya ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa kupitia vijana, kurushiana risasi kwenye ofisi yao binafsi ya faraja trust fund, watu hao wawili wamekanusha madai hayo na kudai yameleta athari kubwa katika familia yao. 



Awali taarifa zilizojitokeza na baadaye kurushwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, ilikuwa ni mama huyo aliyewahi kuwa naibu waziri wa afya, na mwanaye ambaye ni mjumbe wa NEC akiwakilisha vijana, kurushiana risasi kwa kugombea nyumba iliyotaka kuuzwa jijini Dar es salaam.


Hali iliyofanya ITV kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Leonard Paulo ambaye kwa njia ya simu amekiri tukio la mlio wa risasi kujitokeza katika ofisi za faraja, lakini mazingira yake hawezi kuzungumzia hadi arudi ofisini, kwa vile alikuwa safarini.

Hata hivyo Jonas Nkya alipopatikana amekanusha madai hayo na kwamba kilichojitokeza ni kuanguka kwa bastola yake iliyokuwa kiunoni, baada ya kwenda ofisi za faraja kubadilisha gari kwa ajili ya kwenda shamba, ambapo ilijifyetua risasi mbili na kutoa mlio uliosababisha baadhi ya watu kusogea eneo hilo na kwamba kama kungekuwa na ugomvi wa kifamilia, ungefanyika nyumbani kwao ambapo yupo kwa sasa, akimsaidia mama yake kumuuguza baba yake Prof Nkya, ambaye amepooza, madai ambayo yameungwa mkono na mama yake mzazi ambaye naye amehojiwa katika ofisi za faraja, baada ya kukutwa akiendelea na majukumu yake.CHANZO ITV.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: