BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MIAMBA NA VIGOGO WA TANZANIA WALIOTAFUNA MABILIONI BAADA YA KUZICHOTA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW NDIYO HAWA.

HIZI NDIYO BAADHI YA PICHA ZA VIGOGO WALIOTAFUNA MABILION YA FEDHA KUFUATI ZITTO KABWE KUWATAJA BUNGENI KATIKA RIPOTI ILIYOSOMWA.

Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe. Andrew Chenge (Mb) http://www.thisday.co.tz/media/picture/large/DANIEL%20YONA.jpg
Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4.



Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.

Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4

Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4

Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga alipewa shilingi milioni 40.4

Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.

kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4

Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9

Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4

Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62 Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.


Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.


Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4


Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa Tegeta Escrow


Bilioni 73.5 zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006


Taarifa ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa.


Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
NA HAYA NDIO MAPENDEKEZO YA KAMATI
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWAJIBISHWE KWA KUUDANGANYA UMMA WA WATANZANIA - MAPENDEKEZO YA KAMATI YA ZITTO

Filikunjombe: Kamati inashauri kuzitangaza benki za Stanbic na Mkombozi kama asasi za utakatishaji fedha

Filikunjombe: Kamati inashauri bodi ya Tanesco ivunjwe na TAKUKURU iwafungulie mashtaka ya rushwa.

Filikunjombe: Kamati imethibitisha kuwa Naibu waziri wa nishati na madini alisema uongo bungeni naye achukuliwe hatua.

Filikunjombe: Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo amekuwa akisema uongo mara nyingi.

Filikunjombe: Kamati pia imethibitisha kuwa Waziri wa nishati na madini ndiye alikuwa dalali mkuu wa kuunganisha hawa watu

Filikunjombe: Kutokana na sababu hizo hapo juu, kamati inapendekeza kuwa Waziri wa Nishati na madini avuliwe madaraka yake.

Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali utengeuliwe mara moja na aadhibishwe maana ametumia vibaya madaraka

Filikunjombe: Kamati pasipo mashaka imejidhihirisha kuwa Waziri mkuu alikuwa akijua jambo hili ila hakuchukua tahadhari.

Filikunjombe: alisema Mwalimu Nyerere kuwa kumbadili Waziri Mkuu sio jambo la ajabu.

Kwa vyovyote vile, Waziri mkuu anapaswa kuwajibishwa kwa namna yoyote ile ili kurudisha heshima ya serikali maana ameudanganya umma wa Watanzania kwa kusema uongo na kuitete kampuni hewa ya PAP isiyokuwepo

Filikunjombe: Kamati yetu inaamini kuwa Bunge hili litaitumia vizuri taarifa yetu hii

Mh. Spika anna Makinda ameghairisha shughuli za Bunge na kusema kuwa kesho (leo) asubuhi serikali itatoa kauli zake.

Baada ya serikali kutoa kauli zake hapo , Wabunge wengine watapata nafasi ya kuchangia.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: